You can easily invite all your friends to peperonity.com. When you log in or register with us, you can tell your friends about exciting content on peperonity.com! The messaging costs are on us.
NI FAHARI KUMFUKUZA SIMBA AKAKIMBIA,LAKINI NI HATARI KUFUATA NYAYO ZAKE.
Jenga mazoea ya kusoma hadithi ili uongeze maarifa.ifuatayo ni sehemu ya kwanza ya hadithi tamu iitwayo mzee wa shamba,,,endelea.ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti.wahudumu wa chumba hicho walikuwa wamesimamisha shughuli zao zote kwa muda kwa ajili ya kuhudumia maiti mbili ambazo mauaji yake yalimshangaza hata daktari aliyezifanyia uchunguzi.inspekta wabongo nae tayari alikuwa ndani ya chumba hicho,alikuwa akifahamika vizuri kutokana na kufika pale mara kwa mara.bila kusema chochote mmoja wa wahudumu akaifunua moja ya maiti iliyokuwa imefunikwa shuka na kulazwa katika moja ya vya magurudumu,ambavyo ni maalumu kwa kubebea wagonjwa mahututi ama watu waliokufa.pamoja na uzoefu wake wa miaka mingi kazini,na kukutana na mengi ya kutisha zikiwemo maiti za ajabu pamoja na watu waliouawa katika mitindo mbalimbali.staili iliyotumika katika mauaji haya ilimsisimua sana.ilimsisimua kiasi cha kumpa mori wa kufanya kazi kwa nguvu mpya kama kijana anayeanza kazi leo.hakuwahi kufikiria kuwa watu wawili,...itaendelea..